Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwepo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL, Zuhura Muro na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania –  TTC, Mhandisi Peter Ulanga,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Viongozi wengine waliotenguliwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Mabongo na Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania, Maharage Chande,

Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote – UCSAF, Prof. John Nkoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote – UCSAF, Justina Mashiba.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 24, 2024
Wasiowapeleka Watoto shule kuchukuliwa hatua