Mkaguzi Kata ya Tungi Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Mwanamosi Kachule amesema ataendelea kutoa Elimu ya Ukatili kwa kundi hilo ambalo limekuwa likikumbwa na kadhia ya ukatili wa mara kwa mara.

Amebainisha hayo alipotembelea Shule ya awali ya Grace iliyopo kata ya Tungi na kusema kundi hilo litaendelea kupata Elimu ili kuwajengea uwezo watoto wa kupata sauti juu ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanaofanyiwa na baadhi ya wazazi ndugu na walezi na watu wengine katika jamii.

Mkaguzi huyo pia amewataka walimu wa shule hiyo kuwa karibu na watoto hao ili kuIfahamu changamoto wanazopitia watoto hao huku akiweka wazi kuwa endapo walimu hao watakuwa karibu na watoto watapata taarifa nyingi kuwahusu watoto hao na madhira wanayopitia.

Sambambana na hayo Mkaguzi huyo amewaomba watoto hao kusema taarifa zote ambazo wanafanyiwa na watu ili Jeshi hilo liwakamate.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 25, 2024
Dkt. Biteko: Viongozi shirikianeni kuchochea maendeleo