Rais wa Kenya, William Ruto amesema suala kubwa linaloibua hasira kwa Wakenya ni matukio ya ufisadi ambayo yamekuwa yakiripotiwa.

Ruto amesema katika jitihada za kupambana na ufisadi huo atachukua hatua kwa kupendekeza mabadiliko katika sheria za ushahidi.

Amesema, hatua hiyo inalenga kuhakikisha kesi za ufisadi zinachunguzwa na haki kupatikana kwa muda wa miezi sita.

Aidha ameongeza kuwa, wale watakaofichua vitendo  ufisadi watalipwa na kulindwa, ili watu zaidi wajitokeze kuripoti ufisadi.

Tanzania, Comoro wasaini hati za ushirikiano
Habari Picha: Maadhimisho siku ya Mashujaa Mtumba