Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amezindua mradi wa maji wa Real Water uliofadhiliwa na shirika la msaada la kimarekani – USAID, wenye lengo la kuchangia maendeleo katika sekta ya maji Vijijini.

Akizindua mradi huo, Sendiga amesema water mission ni msaada katika jamii kwani  utahakikisha maji yanapatikana kwa uhakika katika maeneo ya Mkoa wa Manyara, kutokana na vifaa ambavyo wameviweka kwa ajili ya kupima na kutibu maji.

Amesema katika Mkoa wa Manyara Shirika la Water Mission limekuwa msaada kwa kuhakikisha mradi huo unaenda kufanya kazi hasa katika Wilaya mbili za Mkoa huo.

Naye Saimon Nkanyemka amesema wana jukumu la kuhakikisha rasilimali za maji zinatekelezwa kwa ubora na kwa uhakika na kwamba mradi utaenda kuwa nq uhakiki wa ubora na usalama wa maji katika maeneo ambayo mradi unatekelezwa hasa maeneo ya Vijijini.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania, Shauri Lazaro amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na salama kwa kushirikiana na RUWASA mkoa wa Manyara kwa kuhakikisha yanapimwa kabla ya kufika kwa mtumiaji.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 27, 2024
Ajali ya Moto: Wanafunzi Lolangulu watolewa hofu