Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, SACP George Katabazi amekabidhi viti mwendo 20 kwa watu wenye uhitaji maalumu, vilivyotolewa na Baraza la Waislamu Mkoa wa Manyara BAKWATA.

Kamanda katabazi amewaomba watumiaji wa hizo viti mwendo wazingatie Sheria za Barabarani kwasababu baiskeli hizo zitakuwa zinatumika Barabarani ambapo kutakuwa na watumiaji wengine, ili waweze kuepukana na ajali.

 

Amesema, Jeshi la Polisi lipo na lina jukumu la  kuwalinda raia na Mali zao lakini ulinzi huo unajumuisha nyanja mbalimbali ikiwemo, Viongozi wa dini, wadau mbalimbali na Taasisi.

Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mohamed Kadidi amewaasa walezi wa watu hao kuwa watunzaji wa viti hivyo, ili kuweza kudumu navyo kwa muda mrefu huku akiwasihi Taasisi na wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kusaidia wenye uhitaji.

Maandamano: Nigeria yahofia kilichotokea Kenya, yawaonya
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 27, 2024