Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatakata wahitimu wa Kozi ndefu ya mwaka 2023/2024 katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), kutumia maarifa waliyoyapata katika kazi zao kwa manufaa yao na nchi zao.
Rais Dkt. Samia ametoa wito huo wakati wa Hafla ya Mahafali ya 12 ya Chuo cha NDC iliyofanyika katika Chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Amesema, wahitimu Watanzania na wa mataifa ya kigeni kutoka nchi 15 kuendeleza ushirikiano ili kuweza kupata suluhu za pamoja katika kutatua changamoto za kidunia kwa utaalam.
Rais Dkt. Samia pia amesema Serikali itaendelea kukiunga mkono chuo hicho, ili kiendelee kutoa michango chanya katika masuala ya kiusalama kitaifa, kikanda na kimataifa.
Aidha, amekitaka Chuo hicho kuendelea kuwekeza kimkakati kwa taifa kwa kuunga mkono tafiti zenye tija na kushirikiana na taasisi zingine za kitafiti ili kuiwezesha nchi kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali.