Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM,  Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa katika Kijiji cha Lupaso mkoani Mtwara, hii leo Julai 28, 2024,

Akizungumza na Wananchi wa Lupaso, Balozi Nchimbi amekiri kuwa yeye ni mwanafunzi wa hayati  Mkapa na amekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), katika kipindi chake na ndiye aliyemlipia ada ya kusoma chuo kikuu akiwalea vizuri wao na Watanzania wote.

Amesema, “alikuwa mzalendo kwa nchi, alifanya mabadiliko makubwa kwa nchi yake na kwa Chama chake, lakini yote CCM chini ya Dkt Samia tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyoacha hayati Benjamin Mkapa. Pamoja hayo nimeambiwa kero za hapa na tumezichukua. CCM inatoa shilingi milioni 10 kuanza kukarabati shule ya hapa Lupaso.”

Katika ziara hii Dk Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amosi Makalla, Katibu wa NEC-Organaizesheni Issa Ussi Haji (Gavu) pamoja na Katibu wa NEC- Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 29, 2024
Othman ahimiza maadili kuvutia jamii ushiriki wa michezo, mazoezi