Klabu ya chelsea imefanikiwa kumnasa golikipa Filip Jorgensen kutoka Villareal ya hispania kwa ada ya euro milioni 20.7 . Golikipa huyo aliicheza mechi 36 kwa msimu uliopita akiokoa michomo 143 sawa na asilimia 69.7 na kufungwa jumla ya mabao 63.
Nyota huyo mwenye miaka 22 alianza kuitumikia timu ya Villareal B akicheza michezo 41 kutoka mwaka 2020 hadi 2023 na baadaye alipandishwa kuitumikia timu ya wakubwa kwa msimu mmoja na kufanikiwa kucheza mechi 38.
Uwezo mzuri aliouonyesha ulipelekea Chelsea kumsajili nyota huyo ili kuongeza ufanisi na ushindani kwa magolikipa Djorde Petrovic na Robert Sanchez. Nyota huyo amesaini mkataba wa miaka 7 ndani ya Chelsea na atakuwa klabuni hapo mpaka mwaka 2031.
Filip amenukuliwa akisema ‘Usajili huu ni ndoto kuwa kweli, nimefurahi sana kusainiwa na Chelsea,hii ni moja ya klabu kubwa sana duniani. Nina shauku ya kumfahamu kila mmoja na kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wenzangu’
Mpaka sasa Chelsea inawawania nyota Aaron Anselmino,Marang Sarr,Alfie Gilchrist,Gabriel Mec ,Karim aDEYEMI kutoka Borrusia Dortmund na Alexander Isak kutoka New castle.