Kuelekea msimu wa 2024/25 Uongozi wa StarTimes umetangaza neema kwa mashabiki wa soka nchini kwa kuwaletea burudani za kutosha kupitia visimbuzi vyake vya antenna na Dish. Startimes imezindua kampeni ya ZOTE NDANI itakayoonyesha ligi zote kubwa duniani ikiwemo BUNDESLIGA,LA LIGA ,ROSHIN SAUDI LEAGUE na CARABAO CUP.
Meneja wa masoko na Maudhui Startimes bwana David Malisa amezindua kampeni hizo na mechi zote zitatangazwa kwa lugha ya kiswahili kupitia chaneli pendwa ya michezo ya TV3 na kusisitiza ubora wa picha ukiwa ni wa High Definition (HD).Chaneli ya TV3 inapatikana kisimbuzi cha antena kwa namba 197 na chaneli namba 131 kisimbuzi cha dishi. pia chaneli hiyo imekuwa ikionyesha michuano mbalimbali ikiwemo AFCON na NBC Championship
Bw.David Malisa amesisitiza kwamba kwa wale wapenzi wa lugha ya kiingereza wakati wa mechi nao hawajaachwa kwani kupitia chaneli za ST World football, SPORTS LIFE hd, SPORTS PREMIUM hd na SPORTS ARENA hd wataweza kuona na kusikia mechi hizo kwa lugha hiyo wakipata uchambuzi kabla ,wakati wa mapumziko na baada ya mechi na zote zitakuwa katika mfumo wa HD
Bw. David Malisa amewahakikishia wadau wa michezo nchini kwamba bei ya vifurushi vyake haitapanda na wataweza kumuona Mbappe na Cristiano Ronaldo kupitia kifurushi cha Mambo kwa shilingi 17000 na kifurushi cha Smart kwa shilingi 23,000 kwa mwezi mzima.