Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii, Subisya Kabuje kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi amesema Watoto walio katika mazingira hatarishi na kaya zao wanapaswa kusaidiwa ili kupata haki zao za msingi.

Ameyasema hayo  alipotembelea katika Taasisi ya SHDEPHA iliyopo Mkoani Shinyanga na kukutana na Kaimu Meneja Mradi Bi. Anitha Aloyce ambapo mbali na majadiliano mbalimbali amewashukuru wadau hao Pamoja nao PACT – ACHIEVE kwa kazi nzuri ya kusaidia ya kusaidia Watoto.

Amesema wadau wanapaswa kushirikiana na Ofisi za Mikoa na Halmashauri ili kufanya usimamizi shirikishi wa Pamoja kwa lengo la kuja na mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kwa makundi yenye uhitaji.

“Kwa kushirikiana na serikali katika vipaumbele vyenu manaweza kuona ni kwa namna gani mnaweza kusaidia katika ujenzi wa nyumba salama (safe house) katika Mikoa ya Kigoma, Tabaro na Shinyanga.”

Aidha Bi. Kabuje ameelekeza wadau hao kwa kushirikiana Ofisi ya Halmashauri kuvipatia mafunzo Vikundi mbalimbali vya kijamii (WORTH yetu) ili waweze kuwa wabunifu wa biashara mbalimbali na kuongeza kipato chao na jamii kiujumla.

Tetesi za usajili Duniani hii leo Agosti 1, 2024
Bandari ya Uvuvi Kilwa kuajiri elfu 30, ujenzi wafikia asilimia 63