Mkaguzi kata ya Parungu Kasera Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Thomas Minza amefanikisha kumrejesha shuleni mwanafunzi Nondo Ramadhani wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mzingi baada ya kupata taarifa katani hapo kuwa kuna kijana ananyimes haki yake msingi yakielimu ambayo wazazi.

Hatua ya Mkaguzi huyo imekuja baada ya wananchi wenye mapenzi mema na Kata hiyo kutoa taarifa za wazazi waliozuia mtoto wao kwenda Shule na kufanya shughuli za Kilimo na uchungaji wa mifugo.

Mkaguzi huyo alibainisha kuwa atopenda kuona kijana wa kata hiyo anakosa elimu akiweka wazi kuwa mazingira ya elimu yameboreshwa ambapo alisisitiza kuwa endapo vijana wa kata yake watakosa elimu watambue kuwa uhalifu utakuwepo.

Sambamba na hayo Mkaguzi wa kata hiyo amebainisha kuwa uamuzi wake umekuja baada ya kupata taarifa hizo ambapo alichukua huamuzi wa kufuatilia suala hilo ambalo limezaa matunda ya mtoto huyo kurejea shuleni na kuendelea na masomo yake ya kidato cha kwanza.

Aidha amewaomba wananchi wa kata yake kuhakikisha vijana wanapata elimu ambapo aliwabia endapo vijana watapata elimu basi watambue kuwa watapata wasomi wengi ambao wataleta maendeleo katani hapo.

Vilevile alisisitiza kuwa endapo vijana watapata elimu watambue fika fikra na mawazo chanya ya maendeleo kwao binafsi na kata hiyo yatakuja kwa kasi na kuwaomba kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wahalifu nauhalifu usiwepo katika kata hiyo.

Bundi wa majeraha atua Man United kabla ya msimu kuanza
Azam FC kuzindua Jezi, Jengo jipya leo