Bodaboda wa kata ya Ngara Mjini Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera wamekubali kutoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, baada ya kupata elimu ya ushirikishwaji Jamii walipokutana na Mkaguzi wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Olipa Chitongo na kubainisha hilo.

Akiongea na madereva hao Chitongo amesema kuwa maafisa usafirishaji hao wakubalina hivyo baada ya kupata elimu hiyo ambao itasaidia katika mapambano ya uhalifu na ukatili katani hapo.

Aidha Mkaguzi huyo amebainisha kuwa kata hiyo inabahati ya kutembelewa na watu mabalimbali ikiwemo wa nchi Jirani ambapo amewaomba madereva hao kutokukubali kutumika vibaya na watu wenye nia ya kuchafua taswira nzuri kata hiyo ambayo imekuwa na sifa nzuri ya amani na utulivu.

Aidha amesisitiza kuwa vijana ndio wanatakiwa kuwa msatari wa mbele katika mapambano ya uhalifu akiwaomba kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana uhalifu katani humo huku akiwa wataka kufuata sheria za usalama Barabarani kuepuka ajali.

Dkt. Biteko amuwakilisha Rais Samia Mkutano mkuu TLS
Dkt.Msonde ataka uadilifu, ufuatiliaji Miradi ya maendeleo