Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amemwakilisha Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Miaka 70 wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).
Mkutano huo, unafanyika hii leo Agosti 1, 2024 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, ukiwa na Kaulimbiu isemayo “Miaka 70 ya kuwepo kwa Tanganyika Law Society”.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Pindi Chana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi, pamoja na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Miaka 70 ya kuwepo kwa Tanganyika Law Society,” na zifuatazo ji picha za baadhi ya matukio mbalimbali.