Klabu ya Simba imemtambulisha rasmi golikipa Moussa Camara anayekwenda kuchukua nafasi ya Ayoub Lakred aliyepata majeraha nchini Misri wakati timu hiyo ikijiandaa na msimu wa 2024/25. Taarifa za ndani zinasema Simba wamefikia hatua ya kumsajiliCamarra baada ya madaktari kudhibitisha kwamba golikipa namba moja Ayoub Lakred atakaa nje kwa muda mrefu.
Historia fupi ya Moussa Camarra.
Golikipa Moussa Camarra alizaliwa novemba 27 mwaka 1998 nchini Guinea. Nyota huyoalianza maisha yake ya kisoka mwka 2014 akiitumikia Milo FC na mwaka 2015 alinunuliwa na Horoya AC ya nchini humo.Nyota huyo aliitumikia Horoya kwa mafanikio makubwa akicheza michezo 37 ya klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho .
Kwa upande watimu ya taifa nyota huyo amechezea timu ya vijana chini ya miaka 17 na 20 na mwaka 2017 alijiunga na timu ya taifa ya nchi hiyo. Kwa sasa ametua Simba na ataitumikia Simba kwa misimu ya 2024/25 na 2025/26. kama ataonyesha kiwango kikubwa basi atajihakikishia kuongeza mikataba mingine ya kusalia klabuni hapo
Hali ya usajili kwa Simba
Mpaka sasa klabu ya Simba ina nyota 13 wa kigeni hivyo kuna uwezekano klabu hiyo ikaachana na nyota Ayoub Lakred na nafasi hiyo kukaimiwa na Camarra. Simba imewaondoa nyota wengi wakongwe waliofanya vizuri msimu uliopita na kuleta wachezaji vijana ili kurudisha hadhi waliyoipoteza misimu mitatu iliyopita/