Baraza la Taifa la Huifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC, Kanda ya mashariki kusini limepiga marufuku matumizi eneo la dampo na machimbo ya mchanga ya eneo la Kiegeani Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kuwa halikidhi vigezo vya utunzaji wa mazingira.

Akizungumza wakati akiwa wilayani Mafia mkoani Pwani kwenye mwendelezo wa ukaguzi wa kawaida Meneja wa NEMC Kanda ya mashariki kusini Lilian Kapakala amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mafia iache mara Moja kutupa takataka katika maeneo ya Kiegeani na kwamba watenge eneo mahusisi kwa ajili ya matumizi hayo ya dampo na machimbo ya mchanga.

Amesema wamekuwa wakiangalia namna ambavyo Sheria ya mazingira ya mwaka 2004 inavyotekeleza na wawekezaji mbalimbali wakiwemo wenye viwanda, hoteli na Halmashauri nchini wazingatie sheria hiyo.

Lilian amesema wakiwa wilayani Mafia wamefanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali yanayotoa huduma kwa Wananchi ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia ambapo upande wa eneo la dampo na machimbo ya mchanga ya Halmashauri ya Wilaya nakubaini maeneo dampo na machimba ya mchanga sio rasmi.

Aidha katika dampo hilo wamekuta takataka zinazotoka majumbani, mahoteli na maeneo mengine ya biashara katika eneo lote la Wilaya ya Mafia ikiwemo plastiki ambazo haitakiwi kutupwa dampo bali zinatakiwa rejereshwe.

Alisema Halmashauri hiyo itoe elimu kwa Wananchi kuhusu utengaji wa takataka kuanzia nyumbani, maeneo ya biashara kwamba taka ziweze kutengwa ili zile za kurejerezwa ziweze kurejerezwa.

Kuhusu mifuko ya plastiki Liliani alisema “Halmashauri ya Wilaya ya Mafia na Wadau wa Maendeleo wa Wilaya hiyo wahakikishe kuanzia masokoni wazingatie kampeni ya katazo la mifuko ya plastiki lifanyiwe kazi na hatutaki kuona tena plastiki wilayani Mafia Wahakikishe plastiki tunazitokimeza wilayani Mafia ili kulinda mazingira yetu,” alisema Lilian.

Alisema eneo hilo la Lipo ndani ya mita 60 kutoka kwenye kolongo la maji ambayo yanapeleka maji ambayo Kuna maeneo mengine yanatumika kwenye umwagiliaji wa mboga na eneo jingine taka hizo zinachomwa jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya katazo la taka ngumu hairuhusu kuchoma takataka kwenye maeneo yetu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Abdul Kitungi alisema eneo hilo lilikuwa ni machimbo ya mchanga na Sasa limenunuliwa na Halmashauri ya Kijiji cha Kiegeani kwa ajili ya ujenzi wa dampo la kisasa ambapo kwa Sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imetenga shilingi milioni 400 kwaajili ya kujenga dampo la kisasa.

“Lakini litakapokuwa tayari tutawaona Wataalamu hususani Wataalamu wa utunzaji wa mazingira NEMC ili tuweze kushauriana nao na kushirikiana nao ili kutunza mazingira wao wakiwa ni Wataalamu wanaotoa maelekezo na sisi tupo tayari kuyazingatia kwaajili ya kulinda na kutetea Sheria na kanuni za utunzaji wa mazingira wa taifa letu” alisema Kitungi.

Dkt. Dugange: Tujitokeze kupiga kura uchaguzi Serikali za Mitaa
Rais Samia azindua Barabara ya Kidatu-Ifakara, Daraja Mto Ruaha