Walimu wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiangalia kwa jicho la tatu Taasisi ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kudai Kwamba watu wameigeuza taasisi kama kampuni yao binafsi na kuichezea, watakavyo huku ikisemekana wanashirikiana na baadhi ya viongozi wa juu.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Agosti 7, 2024 wamesema baadhi ya Viongozi wa Chama hicho wamekuwa wakifanya maamuzi kinyume cha Katiba na Kanuni za Chama Cha Walimu Tanzania (CWT).

Baadhi ya shutuma ni maamuzi ya kuchukua fedha kiasi cha Tsh. Bilioni 2.8 na kuzuia marejesho ya mahali pa kazi bila kuhusisha Baraza la Taifa ambalo ndiyo lenye Mamlaka ya Matumizi ya Fedha na kuzuia Vikao vya Kitaifa kutokufanyika.

“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakuomba Mama yetu ni muumini wa Haki unatupenda Watanzania wote pamoja na Walimu Kilio chetu kikufikie na Mhe. Waziri wa Kazi atasikia na kuhakikisha anatusaidia Walimu wa Tanzania”.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 8, 2024
Ngara: TAKUKURU yaokoa Mil. 4.3 za Wanufaika TASAF