Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wanasiasa kunadi sera za kuwaletea Wananchi maendeleo na siyo kueneza chuki, ubaguzi na uvunjifu wa amani.
Dkt. Mwinyi ameyabaijisha hayo wakati akizungumza na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi na Majimbo ya Mkoa wa Mjini katika Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani na kuwahimiza wanaCCM kuendelea kuhubiri amani kama kipaumbele chao katika mikutano ya hadhara na kujibu hoja zote kwa takwimu.
Amesema suala la mikataba ya bandari Zanzibar na mamlaka ya viwanja vya ndege halijabinafishwa , Serikali imeingia mikataba ya uendeshaji.
Aidha, Dkt. Mwinyi amesema Serikali imetekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa asilimia kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu, masoko, viwanda, michezo, ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wa Serikali na posho zao, pensheni za jamii kwa Wazee na Wastaafu.
Amehimiza pia kuhusu suala la umoja na mshikamano kwa Wanachama wa CCM na kusisitiza kazi ya ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.