Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo August 8, 2024 ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Maabara Kuu ya Kilimo inayojengwa Mji wa Serikali Mtumba Mkoani Dodoma, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 16.
Jengo Hilo la Maabara ya Kilimo lina Ghorofa nne na ndani yake zitakuwepo maabara takribani 14 ambazo zitawawezesha wataalamu na watafiti Nchini kufanya tafiti.