Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakusanya shilingi bilioni 300 kila mwaka ili kulipa madeni na inaweza kulipa deni lolote na bado ni himilivu.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Agosti 8, 2024 wakati  alipokuwa akizungumza na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi na Majimbo za Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa CCM Mkoa.

Amesema, Serikali imeendelea kutekeleza mambo mengi ya maendeleo ambayo wananchi waliahidiwa kupitia ilani ya utekelezaji ya CCM mwaka 2020-2025 na kwamba atajibu kwa takwimu sahihi hoja zote zinazopotoshwa na Wanasiasa.

Dkt. Mwinyi amesema ataendelea kudumisha amani nchini kwa maslahi mapana ya Wazanzibari na kwamba ameidhinisha shilingi bilioni 11 za kulipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa bandari ya Mangapwani.

Rais Samia agawa zana za Kilimo kwa Wizara
Rais Samia atembelea mabanda, aweka jiwe la msingi Nanenane