Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walimbaka na kumlawiti Msichana kisha kusambaza video yake mitandaoni wamekamatwa na Jeshi la Polisi Nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa hii leo Agosti 9,2 024 imeeleza kuwa tukio lilifanyika eneo la Swaswa lililopo jijini Dodoma, Mei 2024.

“Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson,” ilieleza.

Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea ikiwemo kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado hawajapatikana, ili waweze kufikishwa Mahakamani.

Waongoza Watalii watakiwa kulinda maadili ya Kitanzania
Lee Carsley atangazwa rasmi kocha mkuu Uingereza