Naibu waziri Ofisi wa Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Zainab Katimba amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa Kagera kuwa Serikali inaendelea kukabiliana na tatizo upungufu wa watumishi katika kada ya Elimu na Afya baada ya hivi karibuni Serikali kutoa tangazo la ajira hizo.

Katimba ameyasema hayo kwenye mkutano wa hazara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM uliofanyika Agosti 10 katika uwanja wa Mashujaa Bukoba mjini, wakati akijibu kero zilizoibuliwa na wananchi kuhusu tatizo la upungufu wa watumishi katika kada ya Elimu na Afya ambapo amesema Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma na Utawala bora imeshatangaza ajira 9,400 katika kada ya Afya na watumishi 11,000 katika kada ya Elimu na katika idadi hiyo mkoa wa Kagera ni mnufaika wa ajira hizo.

“Mheshimiwa Katibu Mkuu haya ni maelekezo kuwa tutatue changamoto na naomba niwatangazie wananchi wa Bukoba Mjini katika ajira hizi zilizotangazwa muwe na uhakika mtapata mgao wenu wa watumishi katika kada ya Afya na katika kada ya Elimu na mtapata watumishi ili waweze kutoa huduma iliyo bora” amesema

Katimba yupo yupo Mkoa wa Kagera akishiriki ziara ya katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi inayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Ujasiriamali: Vijana Elfu 40 kujikomboa kiuchumi
Rais Samia: Sekta ya Ushirika isimamiwe kwa ukaribu