Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Kilimo kuisimamia kwa ukaribu Sekta ya Ushirika ili uwekezaji unaofanywa na Kilimo, mifugo na uvuvi uweze kufanywa na Vyama vya ushirika.

Rais Samia ametoa agizo hilo katika kikao na Maafisa Ugani na wanaushirika kilichofanyika lkulu, Chamwino jijini Dodoma na kuongeza kuwa Serikali ina dhamira ya kurudisha hadhi ya ushirika hususan ushirika wa mazao hivyo ametaka Ushirika uendeshwe kisasa, uwekezaji ufanywe kitaalam na ukiwa na lengo la kumnufaisha mwanaushirika moja kwa moja.

Amesema, Vyama vya Ushirika vinatakiwa kutokuwa sehemu ya kumyonya mwanaushirika, bali viwe mstari wa mbele kuwalinda na kuwatetea.

Rais Dkt. Samia pia amevielekeza Vyama vya Ushirika kuwa chachu ya mabadiliko na vyenye kuleta mageuzi ya fikra, ikiwemo kuchangia maendeleo mapana kwa kuhamasisha wanaushirika waweze kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote.

Aidha, ameagiza Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika kuhakikisha kuwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali inaleta matokeo makubwa zaidi, kuwafikia wananchi Vijijini pamoja na kuwaelimisha mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt. Samia ameitaka Wizara ya Kilimo kuandaa utaratibu wa kuwapima Maafisa Ugani kwa tija inayozalishwa kwenye Kata au Kiji anachokisimamia ili uwekezaji unaoufanywa na Serikali utoe matokeo yanayotarajiwa.

Hali kadhalika, Rais Dkt. Samia amewataka Maafisa Ugani katika ngazi ya Kata kukaa kwenye vituo vyao na kutumia usafiri ambao Serikali imewapatia kuwafikia na kuwahudumia wananchi.

Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali itaunga mkono juhudi za wanaushirika kuanzisha Benki ya Ushirika ya Taifa kwa kuchangia Shilingi Bilioni 5 kama mtaji ili kuwezesha shughuli za Benki hiyo kuanza.

Ajira Watumishi kada ya Elimu, Afya mbioni
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 11, 2024