Klabu ya Simba imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu ya Kombe la ngao ya jamii baada ya kuifunga Coastal union kwa bao 1-0. Pongezi za kipekee zimwendee kiungo mshambuliaji Saleh karabaka aliyemalizia pasi ya Mukwala.
Katika mchezo huo kocha Fadlu alifanya mabadiliko maeneo matatu,eneo la beki wa kulia alimwanzisha Kelvin kijili badala ya shomari kapombe ,eneo la beki wa Kati alimwanzisha Hamza na eneo la kiungo wa ulinzi alimwanzisha okejepha badala ya mzamiru yassin na Fabrice Ngoma .katika mchezo huo Simba ilianza na wachezaji watatu wazawa ambao ni Mohamed Hussein,Kelvin kijili na omary Hamza.
Matokeo haya yanawafanya Simba waondoke na medali ya Shaba katika michuano hiyo baada ya kushindwa kufuzu hatua ya fainali dhidi ya watani zao wa jadi Yanga mchezo wa nusu fainali waliopoteza kwa kufungwa bao 1-0.