Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa Kombe la Ngao ya Jamii baada ya kuiadhibu Azam FC mabao 4-1. Katika mchezo huo Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Feisal Salum akimalizia pasi ya Gibril Silla dakika ya 14.
Yanga walirudi mchezoni na kusawazisha bao hilo kupitia kwa prince dube dakika ya 18 ,boka akaongeza bao la pili dakika ya 27 na Aziz ki Stephanie akipiga bao la tatu dakika ya 30. Mchezo ulikwenda mapumziko Yanga wakiongoza kwa mabao 3-1.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji mabadiliko hayo yalizaa matunda kwa upande wa Yanga kwani dakika ya 90+3 Clement mzize aliyechukua nafasi ya Prince Dube alipachika bao la nne na kumaliza matumaini ya Azam FC.
Yanga imeuanza msimu wa 2024/25 vyema ikitegemewa kutetea ubingwa wa ligi ya NBC,Kombe la shirikisho la CRDB, na kufanya vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Africa.