Van Persie
Van Persie ameanza kuonja machungu ya kuwa kocha baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi ya Uholanzi (Everidisie) dhidi ya mabingwa watetezi Ajax ,bao likifungwa na Kristian Hlynsson’s.
Van Persie alikabidhiwa mikoba ya kuinoa Heerenveen mwezi julai na anategemewa kufanya maboresho ya kiuchezaji ndani ya timu hiyo. Kocha huyo alijiunga na Klabu hiyo akitokea Feyenoord alikokuwa akihudumu kama kocha wa timu ya vijana ya U18 kwa msimu wa 2023/24.
Wayne Rooney
Mkufunzi wa Plymouth Wayne Rooney amejikuta akipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi ya championship kwa mabao 4-0 dhidi ya Shiffield Wednesday.
Huu ni mwanzo mbaya kwa Wayne Rooney aliyetimuliwa kazi ya kuinoa Birmingham mwezi January mwaka 2024 kwa kuwa na mwenendo mbaya katika mechi 15 na mwezi May 2024 akipata kazi ya kuinoa Plymouth
Wayne Rooney alipewa mkataba wa miaka mitatu mpaka mwaka 2027 na anategemewa kuipandisha timu hiyo ligi kuu uingereza.
Rooney na Van persie waliitumikia Manchester United kwa mafanikio makubwa wakiipa ubingwa wa ligi kuu Uingereza msimu wa 2013. Kwa sasa wote ni makocha na wanatarajiwa kufanya makubwa msimu huu lakini vipigo walivyopata vimeanza kutia doa katika karia zao na mashabiki wao wameanza kuwa na wasiwasi. Swali ni je Rooney na Van persie wanaweza kutupa kile tunachohitaji? Rekodi zao zinaweza kuwa Sawa na Xabi Alonso aliyeiongoza Bayern Leverkusen kutwaa ubingwa wa Bundesliga au kufukuzwa kwa aibu kama Xavi Fernandez? Tuwape muda labda maarifa waliyoyapata kwa Mzee Alex Ferguson yatafanya kazi msimu huu.