Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Mohamed Mchengerwa amepiga marufuku vitendo vya udhalilishaji dhini ya walimu napiga marufuku na kusisitiza kuwa kuanzia sasa nataka aone walimu wakiwa na furaha.
Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kukabidhi magari kwa makatibu wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu yaliyokabidhwa katika mji wa Serikali Mtumba.
Amesema, “sitegemei kuona mwalimu akinyanyaswa mwalimu akionewa kwasababu ambazo mtendaji katika eneo hilo anafanya yenye mwenyewe makusudi, nawataka wakurugenzi wasaidizi, makatibu wasaidizi wa Tume ninao wakabidhi magari leo nendenei mkafuatilie yanayoendelea kwenye maeneo yenu.”
“Kama kuna vitendo vya udhalilishaji dhini ya walimu napiga marufuku kuanzia sasa nataka tuone walimu wakiwa na furaha. Naielekeza Tume kuwa karibu na walimu na kuwasikiliza na kutatua kero zao.
Machengerwa ameongeza kuwa kwa sasa Tume haina visingizio kwani imeshapata bodi na kusisitiza kuwa hataki kusikia mtumishi TAMISEMI ana hofu na serikali yake.
“Wenye zile kero ngumu ngumu wasaidie, sijui uhamisho kwa aliyekidhi vigezi shughulikieni, waliofukuwa washaurini taratibu za kufuata na msijiweke mbali na watumishi. Nimekuwa nikipokea kero nyingi za walimu na kuitaka Tume kujitahidi kuzifanyia kazi kero za walimu kwa haraka,” alisema.
Mchengerwa pia amesisitiza uwajibikaji na kutambuwa majukumu ya kiutendaji kwa watendaji katika maeneo yao ya kazi kwani ndio msingi wa utendajikazi.