Manchester United imekamilisha dili la kumnasa Matthijs De Ligt kutoka Bayern Munich kwa dau la paundi milion 42.Taarifa zilizothibitisha zinasema beki huyo wa kati ameshawasili Carrington kwa ajili ya vipimo na baada ya hapo atatambulishwa rasmi sambamba na beki wa kulia Noussair Mazraoui .

De Ligt mwenye miaka 24 alihudumu ndani ya  Bayern Munich kwa miaka miwili na alifanikiwa kucheza michezo 73 na kufunga mabao matano, nyota huyo alianza maisha yake ya soka Ajax baadaye alinunuliwa na Juventus ya Italy kisha kuuzwa kwenda Bayern Munich.

Manchester United inatakiwa kukamilisha masuala ya kiusajili kabla ya alhamisi ili aingie moja kwa moja kwenye kikosi kitakachocheza siku ya ijumaa dhidi ya Fulham.De Ligt amekuwa kipenzi cha kocha Ten Hag tangu wakiwa Ajax na walifanikiwa kushinda ubingwa wa uholanzi ‘ Eredivisie’ mwaka 2019. Uwepo wa nyota huyo ndani ya United utaimarisha safu ya ulinzi wa kati inayoundwa na Harry Maguire,John Evans,Lennie Yoro ,victor Lindelof na Lisandro Martinez.

Beki Wan Bissaka anaendelea na vipimo katika klabu ya  westham United na kama mambo yatakwenda vizuri basi   Manchester United itapokea kiasi cha paundi milioni 15 kama ada ya kumuuza. Wakati Wan Bissaka akiondoka tayari United wamekamilisha mazungumzo na vipimo kwa mrithi wa beki huyo na tayari wamelipa kiasi cha paundi milion 17 kunasa saini ya  Mazraoui.

Kwanini Matthijis De Ligt atue United?

De Ligt anakuwa beki wa pili wa kati kusajiliwa baada ya Leny Yoro aliyetua klabuni hapo kwa dau la paundi milion 59. Beki huyo alifanya vyema kwenye mechi za kirafiki hasa mchezo dhidi ya Rangers lakini alipata majeraha kwenye mechi ya Arsenal yatakayomweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu hivyo pengo lake linapaswa kuzibwa na mchezaji mwenye uwezo huo ni Deligt.

Victor Lindelof anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu wa 2024/25 lakini pia majeraha ya mara kwa mara ya Lizandro Martinez yamemlazimu Ten Hag kumsajili mchezaji huyo. Beki John Evans umri wake umesogea sana na Harry Maguire si chaguo la kwanza kwa kocha huyo.

TFF yatoa tamko kuhusu mwandishi wa habari aliyeshambuliwa.
Mchengerwa: Sitaki kuona Mwalimu akidhalilika