Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema Matokeo ya utafiti wa nguvu kazi iliyofanyika mwaka 2021, inaonesha kuwa kati ya vijana milioni 14.6 wenye uwezo wa kufanya kazi, vijana milioni 1.8 sawa na asilimia 12 hawana ajira.

Kikwete ameyasema hayo wakati wa Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yaliyofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema “Tatizo la ajira kwa vijana hasa wa kike lipo asilimia 16.7 ukilinganisha na asilimia 8.3 kwa upande wa vijana wa kiume hapa nchini.”

Tuna ziada ya Mchele Tani 1.6 - Baraza la Mchele
TFF yatoa tamko kuhusu mwandishi wa habari aliyeshambuliwa.