Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya kikao kazi katika ofisi ya Wizara ya Maji Mtumba Dodoma na Watendaji wa Sekta ya Maji, ili kuweka mikakati ya utekelezaji wa Mpango Ilani ya Uchaguzi ya kuhakikisha kufikia 2025 Upatikanaji wa Maji mijini unafikia asilimia 95 na Vijijini asilimia 85.
Aidha, Aweso pia ametoa maelekezo mbalimbali, miongozo, mikakati na mipango ya namna gani lengo hili ambalo pia ni kipaumbele chaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika dhamira yake ya kumtua Mama ndoo Kichwani.
Ameyasema hayo alipokutana na uwakilishi makundi yote muhimu ya Wizara ikiwa ni pamoja na baadhi ya wenyeviti wa Bodi, Menejiment ya Wizara na RUWASA, Wawakilishi wa wakurugenzi watendaji wa Mamlaka za Maji na Mameneja wa Mikoa na Wilaya Maji Vjijini (RUWASA) sambamba na Wawakilishi wa Idara na vitengo vyote vya Wizara.
Waziri Aweso pia aliwaalika wataalamu wastaafu wa Wizara hiyo, akilenga kuhakikisha wanatoa mawazo yao ya utekelezaji wa mpango huo, ambapo hali ya upatikanaji wa Maji kwasasa mijini ni asilimia 90 na vijijini asilimia 79.6.