Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba amemtaka mganga mkuu na timu ya usimamizi wa shughuli za Afya wa Halmashauri (CHMT) ya Chato kujitathmini na kuhakikisha wanatoa huduma bora ya Afya kwa Wananchi.
Katimba ametoa maelekezo hayo katika mji wa Chato Mkoa wa Geita, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi Wilayani Chato, Geita.
“Nitafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kwamba mnatimiza wajibu wenu na DMO maelekezo uyapokee na nitafuatilia kwa karibu kuona utekelezaji na tunataka wananchi wa Chato wapate huduma ya Afyayenye ubora kwasababu mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya,” alisema Katimba.
Hata hivyo, maelekezo hayo yanafuatia malalamiko yaliyoibuliwa na Wananchi kuhusu mwenendo usioridhisha wa huduma za Afya.