Mlinzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu wote Nzuguni B jijiji Dodoma, Raphael Ndamanwa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha Mwanamuziki Joseph Francis ‘Mandojo’ kilochotokea Agosti 11, 2024.

Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Anania Amo imeeleza kuwa bado wanaendelea kumuhoji Raphael kuhusu tukio hilo.

Amesema, “tarehe 11 Agosti 2024 saa sita mchana Hospitali ya Rufaa Dodoma, Joseph Michael maarufu kama Mandojo mwenye umri wa miaka 46 Mkurya, alifariki akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.”

Kamanda Amo ameongeza kuwa, “siku hiyo ya tarehe 11 mwezi wa nane saa kumi na moja alfajiri Mandojo alikutwa ndani ya uzio wa Kanisa Katoliki Parokia ya Watakatifu wote akiwa amejificha katika banda la Mbwa, Mlinzi wa Kanisa hilo Raphael Kenneth (26) alisikia Mbwa wanabweka alipokwenda akagundua kuna Mtu amejifungia kwenye chumba kimojawapo.”

“Walifanikiwa kumdhibiti kwa kushirikiana na Waumini wengine, Polisi walifika kwenye eneo hilo na kumpeleka Muhanga Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Jeshi la Polisi linamshikilia Raphael kwa mahojiano na bado uchunguzi unaendelea,” alifafanua Kamanda Amo.

Siasa za machafuko hazikubaliki Tanzania
Watano mbaroni kwa wizi wa Injini 12 za Boti