Klabu ya Coastal Union imewasili nchini Angola kuwavaa Bravo Do maquis kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Africa CCAF. Mchezo huo utachezwa siku ya tarehe 17 Agosti majira ya saa 12 jioni katika dimba la Lubango jijini humo.
Huu unakuwa ni mchezo wa raundi ya kwanza kwa timu hiyo yenye makao yake makuu jijini Tanga , Mchezo wa pili utapigwa jijini Dar es salaam kwenye dimba la Benjamin Mkapa siku ya tarehe 25 Agosti majira ya saa 10 jioni. Kama Coastal Union watavuka hatua hiyo basi watacheza mchezo wa raundi ya pili ambao kama watashinda basi watakwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo ya shirikisho.
Usajili wa wachezaji wapya
ikiwa imesalia siku moja ya kufunga dirisha la usajili Coastal Union imewatangaza nyota wake 13 wapya watakaotumika msimu huu ambao ni Maulid Shabani (MSHAMBULIAJI) Aidan Rasmos (Beki wa kulia) na Jerenie Ntabwe Winga wa kushoto. Nyota hao wanaweza kutumika kwenye mchezo dhidi ya Bravo Do Maquis.
nyota wengine ndani ya kikosi chao ni Hernesi Malonga,John Makwata,Banza Kalumba,Felly Mulumba,Athumani Msekeni ,Haroub Mohammed,Mukrim Issa,Ramadhan Mwenda,Abdallah Hassan naAnguti Luis. Klabu hiyo imesajili jumla ya nyota 12 na kumrejesha mchezaji Felly Mulumba.
Timu hiyo chini ya kocha David Ouma haikufanya vyema kwenye mechi ilizocheza hivi karibuni katika kombe la ngao ya jamii baada ya kufungwa mabao 6 katika mechi hizo mbili huku wao wakifunga mabao mawili pekee. Mchezo wa kwanza dhidi ya Azam FC walifungwa mabao 5-2 na mchezo wa pili walifungwa 1-0 dhidi ya Simba sc. je wamejipangaje na michuano hii ya kimataifa? mwenye jibu kamili ni kocha David Ouma na kikosi chake.