- Klabu ya Azam FC imefanikiwa kuzima uvumi wa kumpoteza kiungo wake Adolf Mtasingwa aliyekuwa akinyemelewa na Yanga. mchezaji huyo alisajiliwa na Azam FC mwezi januari mwaka 2024 na amekuwa akionyesha uwezo mkubwa kila anapopangwa kikosini na jambo hilo liliwavuta mabosi wa Yanga kutaka kumnunua.
Mara baada ya tetesi kuanza kuenea klabu ya Azam FC imeamua kumwongezea mkataba wa miaka mitatu kiungo huyo mwenye miaka 25 na sasa atamaliza mkataba wake na Azam mwaka 2027 hivyo kama kuna klabu imevutiwa naye basi wafike Azam fc kufanya biashara.
Adolf Mtasingwa ni nani?
Adolf Mtasingwa ni jina geni kwenye ligi ya Tanzania. mchezaji huyu ni raia wa Tanzania alizaliwa mwaka 1999 . Nyota huyu hakuwahi kuichezea timu yoyote ya Tanzania kabla hajasainiwa na Azam FC mwezi januari wakati wa dirisha dogo.
Nyota huyu anacheza nafasi ya kiungo mkabaji lakini pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati. mtasingwa amevichezea vilabu mbalimbali vya ligi daraja la tatu nchini ICELAND . Alianza maisha yake ya soka la kulipwa mwaka 2018 katika klabu ya KR Reykjavik na msimu wa 2018/19 alitolewa kwa mkopo kwenda Keflavik kisha kurejeshwa KR Reykjavik msimu wa 2019/20.
Mwezi januari mwaka 2020 alisitishiwa mkataba wake kwa sababu ya janga la corona na mwaka 2021 alijiunga na Volsungur IF alikodumu mpaka januari 13 alipochukuliwa na Azam fc kama mchezaji huru.
Je ataweza kuhimili soka la bongo
Moja ya sifa kuu ya Adolf Mtasingwa ni utulivu nyakati zote anapokuwa uwanjani,kiungo huyu ni mwepesi wa kusoma mchezo na kubadilika, mbunifu na anauwezo wa kukaa na mali miguuni. mara zote amekuwa akibadilika kulingana na aina ya wapinzani anaocheza nao. Kurejea kwa Sospeter Bajana kutaleta muunganiko mzuri baina yao na itarahisisha kazi kwa kiungo wa ushambuliaji James Akaminko. Ikumbukwe Adolf ameshacheza baadhi ya mechi za ligi ya NBC tangu januari hivyo tutegemee makubwa kutoka kwake msimu ujao.