Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Nchini- RCT, Geoffrey Rwiza amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bei ya Mchele ili Wakulima wapate tija katika kilimo cha mpunga.
Amesema hayo wakati akizungumza na Wakulima wa mpunga kwenye mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Mchele Wilayani Mbalali mkoani Mbeya.
Amesema Baraza la Mchele Tanzania – RCT, Wana haki ya kumshukuru Rais Dkt Samia kwa jitihada anazofanya kuwasaidia Wakulima wa mpunga nchini ambapo hivi karibuni ameagiza kuongeza bei ya Mchele ili kuwakwamua Wakulima wa mpunga wapate tija.
Amesema Rais amefanya jitihada katika kuwasaidia Wakulima nchini ambapo sasa mpunga unazalisha kwa kiasi kikubwa sana hadi Sasa tuna ziada ya Mchele tani zaidi ya milioni 1.6 .
Rwiza alisema Serikali’ imetoa uwezeshaji wa skimu za umwagiliaji, ruzuku ya mbolea, Maafisa ugani wamewezeshwa kusaidia Wakulima ndio maana Wakulima wameweza kufanikiwa kupata mavuno mengi zaidi.
“Tunashukuru kwaajili ya jicho la kuona adha waliyokuwa wakipitia Wakulima hata kuongeza bei ya Mchele itakayowapa tija Wakulima maana tulikuwa tunazalisha na kuuza Mchele kwa bei ya hasara kwani gharama za uzalishaji bado zipo juu,” alisema Rwiza.
Afisa Sera na uchechemuzi wa Baraza la Mchele Tanzania RCT Leoncia Salakana amewataka Wakulima wadogo kuzingatia kilimo biashara bora kulima katika eneo dogo na kupata mavuno mengi.
Naye mwana kundi wa Safi cha Kijiji cha Mabadaga wilayani Mbalali mkoani Mbeya Mariam Wakuganda ameomba usajiri wa Wakulima wa mpunga uwe endelevu ili vijana wanaomaliza elimu ya msingi waweze kusajiriwa waendelee kunufaika na mbolea na ruzuku za Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa kongami ya Mbegu ya mpunga Mkoa wa Mbeya, Imani Makanyaga ameomba Serikali’ kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mbalali kuongeza wazalishaji wa Mbegu ili kuwatosheleza Wakulima nchini.