Ligi kuu ya NBC inaanza rasmi tarehe 16 Agosti na vilabu 16 vipo tayari kuanza safari ya kuwania ubingwa wa ligi hiyo. Tumeshuhudia timu zote zikifanya sajili za wachezaji wapya na makocha na baadhi ya wachezaji na makocha wakiachwa yote kwa yote ni katika kuboresha timu zao.

Ushindani wa ligi hiyo ni mkubwa mno msimu huu maana kila ukisoma vikosi vya kila timu unaona ni majina makubwa ya wachezaji na wengi ni wazoefu wa kusakata kabumbu.Swali pekee unaloweza kujiuliza ni je wachezaji hao wataonekana katika viwanja vipi? na je ni viwanja gani bora vinavyoongeza thamani ya ligi yetu.

Viwanja vitano bora vitakavyotumika msimu huu ambavyo vimekarabatiwa na kuwa vya kisasa kabisa.

1.AZAM  COMPLEX -Dar es salaam 

Uwanja huu ni mali ya Azam FC,kipindi ambacho ligi ilisimama uongozi wa klabu hiyo ulifanya maboresho katika eneo la kuchezea,maboresho ya majukwaa kwa kuwekwa viti na kuufanya ukidhi vigezo vya CAF. Uwanja huu utatumiwa na vilabu vya Azam FC na Yanga kwa mechi za nyumbani.

 

2.KMC COMPLEX- Dar es Salaam

Uwanja huu unamilikiwa na manispaa ya Kinondoni na upo katikati ya jiji la Dar es salaam eneo la Mwenge. Huu ni uwanja mpya wa kisasa ambao haujawahi kutumika kwenye mechi za ligi.Uwanja huu ulikabidhiwa kwa klabu ya KMC na utatumika kwa mechi zake 16 za nyumbani. Uwanja huu haubebi mashabiki wengi ila umeboreshwa eneo la kuchezea. `Klabu ya Simba itautumia uwanja huo kwa mechi zote za nyumbani.

3.MAJALIWA STADIUM – Lindi

Uwanja wa Majaliwa Stadium ni moja ya viwanja vikubwa kwa uwezo wa kubeba mashabiki na umekuwa ukitumika kwa msimu wa tatu mfululizo. sifa kubwa ya uwanja huo ni kuwa na eneo zuri la kuchezea lililowekwa nyasi bandia. Uwanja huu hutumika kwa mechi za mchana na usiku. Uwanja huu unamilikiwa na kuendeshwa na klabu ya Namungo.

 

4.Kaitaba Stadium – Bukoba 

Huu ni uwanja bora zaidi kwa kanda ya kaskazini.Uwanja huu unamajukwaa machache lakini unasifa za kipekee ikiwemo eneo zuri la kuchezea likiwa na nyasi bandia pamoja na taa zinazouruhusu uwanja huo kutumika kwenye mechi za usiku. Mashabiki wa kagera sugar wamekuwa wakifurahishwa na namna timu yao ikisakata kabumbu la hali ya juu wanapokuwa nyumbani.

 

5.CCM KIRUMBA- MWANZA 

Pamba jiji wanautumia uwanja wa ccm kirumba uliopo jijini mwanza kwa mechi zake za nyumbani, uwanja huu ni mkubwa wenye kubeba mashabiki wengi zaidi kuliko viwanja vingine vilivyotajwa hapo juu ,uwanja huu umeboreshwa eneo la kuchezea hivyo tutegemee kutoleta usumbufu kipindi cha majira ya mvua. 

 

 

 

Viwanja vya Benjamini Mkapa na Uhuru havimo kwenye orodha hii kwasababu vipo katika ukarabati mkubwa.Benjamin Mkapa utatumika kwenye mechi za Simba vs Yanga,Azam vs Yanga  na Azam vs Simba.

Baada ya kuwabwaga Chelsea: Pochettino apata shavu marekani
Tabora na Biashara United zatolewa kifungoni