Timu ya taifa ya Marekani imemtangaza rasmi Kocha Mauricio Pochettino kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kuelekea michuano ya kombe la Dunia mwaka 2026 . Marekani ,Canada na Mexico zitaandaa michuano hiyo mwaka 2026 na chama cha soka Marekani kinaamini uwepo wa kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Tottenham kutairejesha timu kwenye hali ya ushindani.
Mauricio Pochetino aliachana na Chelsea mwezi june 2024 baada ya kuiongoza timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja akitokea PSG. Kocha huyo amewahi kuvifundisha vilabu mbalimbali vikiwemo Espanyol ya hispania kuanzia mwaka 2009 hadi 2012 kisha akahamia Southhampton alikodumu kwa mwaka mmoja na kuelekea Tottenham mwaka 2014 alikodumu hadi mwaka 2019. Akiwa Totenham alifanikwa kuiongoza timu hiyo kwenye mechi 293 na baadaye alielekea PSG alikodumu kwa miezi 15 akiiongoza timu hiyo kwenye michezo 84.
Kocha Mauricio Pochettino anafaa kupewa majukumu ya kuiongoza timu hiyo ya taifa kutokana na uwezo wake wa kuinua vipaji vya vijana. Tumeshuhudia namna kocha huyo alivyoboresha viwango vya akina Son na Harry Kane kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 na kama atapewa uhuru wa kimajukumu basi ataboresha timu ya taifa ya Marekani.