Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa- UNESCO, limesema Wasichana wanaokaribia milioni 1.4 wamenyimwa fursa ya kupata elimu ya sekondari nchini Afghanistan.

Shirika hilo limesema unyimwaji wa haki hiyo umetekelezwa tangu utawala wa Taliban uliporejea madarakani mwaka 2021, hatua ambayo inaweka hatari kwa kizazi kijacho kielimu.

Taarifa ya Shirika hilo pia imeeleza kuwa wakati hii leo utawala wa Taliban ukifikisha miaka mitatu madarakani, idadi ya Wasichana wanaojiunga na shule ya msingi nchini humo pia imepungua.

Aidha, sichana karibu milioni 2.5 waliozuiwa haki ya kupata elimu, wanawakilisha asilimia 80 ya wasichana walio katika umri wa kusoma kwenye taifa hilo ambalo wanawake wanakabiliwa na vizuizi.

Afghanistan ndio taifa pekee ulimwenguni ambalo lililozuia Wasichana na Wanawake kusoma Sekondari na Vyuo vikuu.

Wakutana kujadili mabadiliko mikataba ya uongozi EAPP
Baada ya kuwabwaga Chelsea: Pochettino apata shavu marekani