Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumchukulia hatua kali za kinidhamu Afisa Ardhi Mwandamizi Gaudence Mtalo kwa kusababisha mkanganyiko kwa kukosa uadilifu katika kutekeleza majukumu yake.

Waziri Ndejembi ametoa maelekezo hayo jijini Dar es salaam wakati wa kikao chake na Watumishi wa Ardhi Mkoa wa Dar es salaam na Pwani baada ya kusikiliza pande mbili zinazodai kumiliki kiwanja kilichopo Tegeta Wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam ambacho mtumishi huyo anahusika katika mkanganyiko huo.

“Hatuwezi kuvumilia tabia za namna hii, ninyi ndiyo mnatuletea matatizo ya kuichafua Wizara, huu mkanganyiko umesababishwa na Afisa asiye mwadilifu na ndiyo wanatusababishia migogoro mingi, Afisa asiyefuata taratibu sisi hatuwezi kumvumilia.”

“Naelekeza ukaripoti ofisi za TAKUKURU, ili uelezee umefikiaje maamuzi haya ya kutofuata taratibu lakini pia Katibu Mkuu akuchukulie hatua za kinidhamu,” amesema Ndejembi.

Maboresho kanuni CSR kuleta ushirikiano wa jamii, Makampuni.
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 16, 2024