Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, limetaka kuongezwa kwa uzalishaji wa chanjo ya kipindupindu kutokana na upungufu mkubwa wa hitaji hilo uliwenguni.

Kupitia andiko la mtandao wa X, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tayari hadi kufikia Julai 28, 2024 visa 307,433 vya kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa katika mataifa 26.

Hata hivyo, tayari Nchi 18 zimeagiza dozi milioni 105 tangu mwezi Januari, lakini ni dozi milioni 55 tu zilizotengenezwa na hivyo kuona upo umuhimu wa kuongeza juhudi zaidi kuhakikisha suala hilo linatiliwa mkazo.

Aidha, WHO pia imesisitiza uwekezaji zaidi utakaosaidia kuongeza uzalishaji wa chanjo na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na usafi, ili kuzuia milipuko zaidi ya kipindupindu unazingatia.

TNGP: Wapeni nafasi msiwasukumie kwenye viti maalum
Maboresho kanuni CSR kuleta ushirikiano wa jamii, Makampuni.