Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania – TGNP, Lilian Liundi amevitaka Vyama vya siasa kutowalazimisha Wanawake kugombea nafasi za viti maalum.
Lilian ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Makatibu wa vyama vya siasa ngazi ya kata kutoka vyama mbalimbali vya siasa, wanaoshiriki mafunzo ya umuhimu wa ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi, katika ukumbi wa mikutano wa TGNP.
Amesema, “tunaomba sana mkawape wanawake nafasi, muwatie moyo, wanapokuja kuchukua fomu msiwasukume kwenye viti maalum, wapeni nafasi waende kwenye viti vya kundi la wajumbe mchanganyiko, wagombee pia uenyekiti wa mitaa na vijiji.”
Lilian poa amewataka Makatibu wa vyama ngazi ya Kata kuhakikisha Wananchi ambao wapo kwenye maeneo yao wanashiriki kutoa maoni kwenye dira ya Taifa 2050, ili waweze kutoa maoni ya mwelekeo wa taifa kwa miaka 25 ijayo.