Christian Eriksen ameambiwa na Manchester United kwamba anaweza kutafuta klabu nyingine, Erik ten Hag hana mpango wa kuungana na Frenkie de Jong, Atletico wana muda ambao wangependelea Joao Felix kuondoka na Conor Gallagher kuwasili kutoka Chelsea.

Manchester United wamemwambia kiungo wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, 32, kwamba yuko huru kutafuta klabu mpya mwezi huu na anaweza kuondoka kwa mkataba wa bei nafuu. (Football Insider)

Manchester United hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 27.(Metro)

Atletico Madrid inalenga kukamilisha mauzo ya mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, mwenye umri wa miaka 24 kwa Chelsea na kumsajili kiungo wa kati wa The Blues mwenye umri wa miaka 24 Conor Gallagher ifikapo Jumatano. (AS – kwa Kihispania)

Conor Gallagher

AC Milan wamefikia makubaliano na Monaco kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Youssouf Fofana, 25, ambaye pia ananyatiwa na Manchester United. (Anga Italia)

Manchester United wanaendelea kujadiliana na Burnley kuhusu mkataba wa kiungo wa Norway Sander Berge, 26. (Sky Sports)

Vilabu vvya Stoke City, Swansea City na Oxford United vina nia ya kumsajili beki wa wa Scotland Max Johnston mwenye umri wa miaka 20 kutoka Sturm Graz. (Football Insider)

Union Berlin na Getafe wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Cameron Archer, 22, kwa mkopo kutoka Aston Villa. (Fabrizio Romano)

Chelsea wameweka bei ya £60m kwa klabu yoyote inavyotaka kumsajili winga wa Uingereza Noni Madueke, 22. (Athletic – usajili inahitajika)

Beki wa zamani wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 34, “angependa kujiunga” na Manchester United baada ya kuwa mchezaji huru alipondoka Barcelona. (Fabrizio Romano via Givemesport)

Paris St-Germain iko tayari kuipiku Chelsea katika usajili wa kiungo wa klabu ya Rennes ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 23 Desire Doue. (ESPN)

Alonso amekuwa mchezaji huru alipondoka Barcelona.

Chanzo cha picha,Getty Images

Everton wanajadili uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Napoli na Uswidi Jens Castuje, 25. (TeamTalk)

Brighton wamewasilisha ofa iliyoboreshwa kwa mlinzi Olivier Boscagli mwenye umri wa miaka 26 – ambaye aliichezea timu ya vijana ya Ufaransa – lakini bado haitoshi kwa PSV Eindhoven. (Voetbal International – kwa Kiholanzi)

Watoto waokota bomu, saba wafariki
Maajabu: Kutana na Soko la Watu waliokata tamaa