LA LIGA YAANZA RASMI

Ligi kuu nchini Hispania imefunguliwa rasmi hapo jana kwa mechi mbili zilizowakutanisha Athletic Club dhidi ya Getafe na mchezo wa pili uliwakutanisha Real Betis dhidi ya Girona. Mechi zote zilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Ligi hiyo itaendelea siku ya leo kwa kuzikutanisha klabu za Celtavigo dhidi ya Deportivo Alvales majira ya saa 8;00 usiku  na mchezo wa pili utapigwa saa 10:30 kwa kuwakutanisha Las Palmas dhidi ya Sevilla. La Liga imesheheni nyota mbalimbali waliofanya vyema kwenye michuano ya Euro na Olympic. Kylian Mbappe aliyetua Real Madrid msimu huu ameongeza mvuto wa ligi hiyo na mashabiki wanaamini atakwenda kuvunja rekodi zilizowekwa na Cristiano Ronaldo pamoja na Lionel Messi. Usajili wa Juan Alvarez kutoka Manchester City kwenda Atletico Madrid umeongeza thamani ya ligi hiyo.

EPL KUREJEA LEO 

Ligi kuu Uingereza inafunguliwa rasmi leo kwa kuzikutanisha klabu za Manchester United dhidi ya Fulham mchezo utakaopigwa majira ya saa nne kamili dimba la Old Trafford . Mchezo huo muhimu kwa timu zote mbili na utatoa picha halisi kwa United kwa msimu. Mmiliki mpya wa klabu hiyo Bw. Ractiff ameiweza  kufanya sajili za mabeki watatu wenye thamani ya paundi milioni 112 pamoja na straika Joshua Zirkzee mwenye thamani ya paundi milion 36.Matumaini mapya yamerejea klabuni hapo na wengi wanaamini ni wakati sahihi kwa klabu hiyo kurejesha makali yake

Simba yafunga dirisha la usajili kwa kishindo
Maisha: Hii hapa dawa ya matapeli wa Viwanja