Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake, Florent Kyombo imeanza kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu Miswada minne (4) ya Sheria.
Kamati hiyo inapokea maoni ya wadau kuhusu Miswada iliyosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Nne (14) na 15 wa Bunge. Miswada hiyo ni pamoja na;
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania (The Law School of Tanzania (Amendment) Act, 2024).
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2024);
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Bill, 2024); na
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (The Prevention and Combating of Corruption (Amendments) Bill, 2024).
Wadau kutoka Asasi za Kirai takribani Kumi (10) walifika kutoa maoni yao wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Watetezi wa Haki za Wanawake, Mtandao wa Kupinga Rushwa ya Ngono na Ustawi wa Mtoto wa Kitanzania.
Vikao vya kupokea maoni ya Wadau vinategemewa kuhitimishwa kesho leo Agosti 16, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.