Katibu Tawala Msaidizi (Seksheni ya Utawala na Rasilimali Watu) John Tilubuzya amewataka Washiriki wa mafunzo ya mpango wa Shule Salama kutumika kama kichocheo cha mabadiliko chanya katika sehemu zao za kazi kupitia maarifa na mbinu watakazopata katika mafunzo ya Mpango wa Shule Salama.

Tilubuzya amesema hayo alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo maalum yanayowahusisha washiriki kutoka Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara yakilenga kuwajengea uwezo washiriki ili kuhakikisha shule za sekondari zinatoa elimu bora kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyowakabili wanafunzi.

Amesema, “tunategemea kupitia Mafunzo haya mnayopata kila mshiriki kwa nafasi yake ataweka mazingira Salama Shuleni na kuongeza Usalama wa watoto wetu kwa jumla. Naamini mpo katika mafunzo haya si kwa bahati bali mnastahili na lengo la Mafunzo haya litafanikiwa kwa kiasi kikubwa.”

Mafunzo hayo maalum ya Siku tatu yanahusisha wenyeviti wa bodi za shule za sekondari, maafisa kutoka ngazi za mikoa, maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya mkoa, pamoja na waratibu wa Mpango wa Shule Salama.

Waomba mapigano yasitishwe kupisha chanjo kwa Watoto
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 17, 2024