Wakubwa wanasema ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii na tukio la kuanzishwa kwa ndoa huitwa harusi, ila kabla ya ndoa kuna kipindi cha uchumba ambapo wawili waliokubaliana huchunguzana tabia na kujifunza au kujuana zaidi kabla ya kufunga pingu za maisha na kama wawili hao wataamua kukomesha ndoa yao kisheria, hiyo huitwa talaka.

Kimantiki karibu kila Taifa Duniani huwa na utaratibu wake wa kisheria katika mambo ya ndoa, ambapo wahusika (Wanandoa), huufuata na inakuwa upo kisheria na iwapo itatokea mtafaruku baina yao basi utakuwa ndiyo mwongozo wa nini cha kufanya, ili kuwapatia muafaka.

Taratibu hizi, mara nyingi huwa zinafanana kwa baadhi ya maeneo mbalimbali Duniani lakini kule Nchini Dominica mambo ni tofauti kidogo kwani walipitisha sheria kuwa, Wanandoa kabla hawajafunga ndoa ni lazima wakubaliane ni kiapo kipi wanataka kuapa.

Ipo hivi, kama Wanandoa baada ya kukubaliana kimaisha wanatakiwa kutumia moja ya aina tatu za viapo ambavyo vimepitishwa kisheria kwa kutumia kiapo kitakachosimamiwa na wafungisha ndoa katika nyumba za ibada au Serikali na kuchagua (i). Kuishi kwenye shida na raha, (ii). Kuishi kwenye raha tu na (iii). Kuishi kwenye shida tu.

Taifa hilo, liliamua kutunga sheria hiyo baada ya kugundua kuwa kwenye ndoa za sasa usaliti na ugomvi umekithiri na unasababisha familia kukosa furaha kila siku na kwamba wengi wao hufika kufungua mashitaka ya kuachana wakilalamikia mambo ambayo katika viapo walikubaliana nayo lakini wameshindwa kuyaishi, hivyo kuleta utata.

Wengi wameifurahia sheria hiyo hasa Wanaume na sasa endapo mmoja wa Wanandoa ataenda Mahakamani kwa mgogoro wa ndoa, basi kesi yake itaamuliwa kutokana na kiapo alicho kubaliana na mwenza wake siku ya ndoa, yaani kama walikubali kuapa watakua pamoja kwenye shida na kilicho kupeleka mahakamani ni shida basi hapo hakuna kesi.

Halafu kama mmoja wa Wanandoa alikubali kuishi kwa raha tu, lakini kakuta shida basi akienda Mahakamani ndoa hiyo itavunjwa rasmi kwakua kiapo kinakinzana na uhalisia alioukuta na kama aliapa kwa shida na raha basi akikutana na ndivyo sivyo au vyote kwapamoja na bado analalamika basi imekula kwake.

Ajali Kiwanda cha Mvinyo yawapa darasa akina pangu pakavu
Uviko-19, Vita chanzo umasikini wa Mataifa 10 Duniani