Inaarifiwa kuwa mwaka 1875 huko Dublin nchini Ireland, katika Kiwanda kimoja cha Pombe aina ya Whisky, kulitokea hitilafu iliyosababisha moto mkubwa.
Jambo la kusikitisha ni pale ambapo katika tukio hilo watu takribani 13 walipopoteza maisha lakini kati ya hao hakuna aliyekufa kwa kuungua moto.
Taarifa zinasema wote walikufa kwa sababu walikunywa pombe nyingi iliyokuwa ikitiririka mitaani baada ya mapipa takribani 5000 ya Pombe kupasuka.
Ama kweli kufa kufaana iliacha majonzi kwa familia nyingi baada ya tukio hilo, ambalo limeacha historia na alama katika mioyo ya walioondokewa na wapendwa wao.