Baraza la Mchele Tanzania – RCT, limeiomba Serikali na Wadau wa elimu kuwekeza kwenye tafiti ndogo ndogo za zao la Mpunga kuanzia elimu ya Sekondari hadi vyuo vikuu, ili kurithisha ujuzi na uzoefu wa kuendeleza Kilimo hicho nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mchele Tanzania RCT Geoffrey Rwiza kwenye mkutano wa Jukwaa la Wadau wa Mchele Wilayani Mbalali mkoani Mbeya.

Amesema, Wanafunzi shuleni hufanya miradi maalumu ya tafiiti za kimafunzo kwa Wanafunzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wapate ujuzi ili waendeleze kilimo cha mpunga nchini hapo baadae.

Rwiza ameongeza kuwa Wanafunzi waelekezwe kufanyia tafiti zao hilo la mpunga ili isaidie kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakulima wa mpunga nchini.

Amesema, “lakini pia kuwatamanisha Wanafunzi kuwa na hamu na kiu ya kuhudumia sekta ya Mchele”Waje huku nako wafanye tafiiti wakiwa kidato cha nne ili wakifika kidato cha tano na sita hadi kikuu wawe na uelewa mkubwa wa zao la mpunga.”

Yanga yaisambaratisha Vital'o Ligi ya Mabingwa Africa
Ajali Kiwanda cha Mvinyo yawapa darasa akina pangu pakavu