Vilabu vya Manchester United, Liverpool,Arsenal na New castle vimeanza vyema ligi kuu ya Uingereza baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo hiyo.

Manchester United

Manchester United dhidi ya Fulham ndiyo iliyofungua ligi hiyo mchezo uliopigwa dimba la Old Trafford.katika mchezo huo United waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji mpya Zirkzee dakika ya 87. Kocha Erik Ten Hag alinukuliwa akisema usajili wa wachezaji wanne walioufanya utawapa matokeo chanya msimu huu.

Liverpool

Kocha Arne Slot ameanza rasmi kibarua cha kuiongoza Liverpool kuelekea ubingwa wa ligi kuu Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-O dhidi ya Ipswich. Diego Jota alipachika bao la kuongoza dakika ya 60 na Mohammed Salah alishindilia ushindi huo kwa bao la pili dakika ya 65.

Arsenal

Klabu ya Arsenal imeanza vyema baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-O dhidi ya Wolves. Kai Havert alifungua dirisha la mabao dakika ya 25 akimalizia pasi ya bukayo saka na bao la pili lilifungwa na Bukayo Saka mwenyewe.Huu ni mwanzo mzuri kwa kocha wa klabu hiyo Mikel Arteta aliyeshindwa kutwaa ubingwa wa EPL mara mbili mfululizo mbele ya Pep Guardiola wa Manchester city.

Brighton Halves

Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton unawafanya Brighton kuongoza  msimamo wa ligi kuu uingereza kwa mechi zilizochezwa.

Huu hapa msimamo wa ligi hiyo

 

Yusuph Kitambi awaponza Tabora United
Yanga yaisambaratisha Vital'o Ligi ya Mabingwa Africa