Baraza la Mchele Tanzania – RCT limeomba serikali kusaidia kuondoa vikwazo vidogo vidogo vya kibiashara katika soko la Mchele la nchi za Afrika Mashariki ili mchele wa Tanzania uuzwe katika nchi hizo Wakulima na taifa lipate kipato chenye tija sawa na makubaliano ya jumuhia hiyo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mchele Tanzania RCT Goefrey Rwiza wakati akizungumza katika Jukwaa la Wakulima wa mchele wa mkoa wa Iringa ambapo Baraza hilo lipo katika ziara ya kutembelea na kuzungumza na viongozi wa majukwaa ya wakulima wa Mpunga katika Majukwaa 11 ya wakulima wa mpunga nchini.
Amesema serikali iendelee kuwasimamia soko la mchele katika nchi za Afrika Mashariki kwani kuna makubaliano ya nchi za Afrika Mashariki kuhusu Kodi ya mchele unaotoka nje ya nchi za Afrika Mashariki kuingia katika nchi zetu ambayo yanasimamiwa na jumuhia ya Afrika Mashariki katika kutafuta mstakabali mzuri wa sekta ya mchele katika nchi zake.
Rwiza amesema Baraza hilo linashukuru serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulinda makubaliano ya awali ya jumuhia ya muungano wa Afrika Mashariki ya kutoza asilimia 75 kwa mchele unaoingia nchini ambayoi hufanya mchele kutoka nje kuwa na bei kubwa kuliko mchele wa ndani ya nchi.
Bahati mbaya nchi zingine za afrika mashariki wamepunguza kwasababu mbalimbali kwani Kenya wamepunguza hadi kufikia asilimia 35, Uganda wamepunguza hadi asilimia 45 lakini kwa upande wetu tunaona serikali yetu inaendelea kuilinda sekta ya Mchele kwa gharama kubwa”
“Kwa Mfano mchele kutoka Tanzania hautakiwi kulipa kodi yoyote kwenye nchi yoyote ya Afrika Mashariki kadhalika mazao mengine yote ya kilimo yanatakiwa kwenda bure lakini ukienda Uganda wanatoza VAT mchele wetu sisi tukienda kulalamika wanasema VAT sio suala la Jumuhia ya Afarika Mashariki ingawa makubaliano ya awali ni kwamba nchi zetu zisitoze kodi na sisi sidhani kama kuna mazao yoyopte kutoka nchi hizo kama yanalipiwa VAT”
“Sasa mchele wetu kwenda Uganda unatakiwa kulipiwa VAT na Kenya nao wameanzisha ni kama kodi ambayo ni kikwazo cha Kibiashara kwamba mchele wetu tuupeleke kupimwa maabara ili kuthibitishwa kama una vinasaba vya mbegu bora za kisasa kwa gharama kubwa jambo ambalo tunaliona kama ni kikwazo cha kibiashara”
“Pia nchi ya Kenya wameruhusu tani laki tano kuingia nchini mwao kutoka nchia ambazo sio za jumuhia ya Afrika Mashariki ambao unauzwa kwa gharama ndogo hivyo mchele wetu Tanzania unakuwa bei ya juu”
“Jambo jingine ni vikwazo vya mipakani gharama zinakuwa kubwa kwani magari yanasimamishwa kwasababu ya vikwazo mbalimbali vinavyoongeza gharama na kusababisha mchele wetu un akuwa bei kubwa na kukwamisha kufanya biashara”
“Serikali yetu kupitia jumuhia ya Afrika Mashariki iendelee kusimamia mchele wetu uende katika hayo mataifa na kuuzwa bila vikwazo vya aina yoyote kwani katika ile ziara ya mchele katika taifa ya zaidi ya tani milioni moja na nusu wao ni wanaohusika wa kubwa kununua”.
Alisema iwapo itasimamiwa vizuri mchele utaweza kuuzika vizuri kwa kasi kubwa na wakulima wataweza kulima kwa nguvu ya kulima zaidi na kuingiza kipato kikubwa kwa serikali na kwa Wakulima.