Klabu ya Azam fc imeanza vyema mbio za kufuzu hatua za makundi ya ligi ya mabingwa Africa kwa ushindi wa mabao 1-0.Azam walipata bao la kwanza dakika ya 56 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Blanco baada ya Feisal Salum kuchezewa madhambi eneo la hatari.
Mchezo huo uliojaa ufundi mwingi ulipigwa dimba la Azam Complex na Kocha Yusuf Dabo aliupania mchezo huo kwa kumuanzisha Mohammed Mustafa eneo la golini akilindwa na mabeki wanne ambao ni Pascal Msindo,Yannick Bangala, Pablo Fuentes na Lusajo Mwaikenda. Eneo la kiungo liliundwa na James Akaminko,Mtasingwa,Gibril Silla, Tiesse na Safu ya ushambuliaji iliongozwa na Feisal Salum akisaidiana na Blanco. Azam waliutawala mchezo huo kwa vipindi vyote viwili na kuwafanya APR kucheza kwa kujilinda nyakati zote .
Azam walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Adam Adam pamoja na Iddi Nado.Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Azam FC alinukuliwa akisema Matokeo haya yanawafanya kujiamini na kucheza kwa mbinu wanazozitumia kila wakati kuelekea mchezo wa marudiano jijini Kigali nchini Rwanda tarehe 25 Agosti.